Jumatatu 25 Agosti 2025 - 23:19
Mjumbe Mwandamizi wa Hizbullah: Uamuzi wa Serikali wa Kutaifisha Silaha za Muqawama ni Hatari na Unaweza Kuliweka Taifa Kwenye Ukingo wa Mlipuko

Hawzah/ Sheikh Ali D’amoush amesisitiza kwamba uamuzi wa kijinga ambao serikali imechukua wa kutaifisha silaha za Muqawama si tu kwamba umekosea sehemu ya kanuni, bali pia umelikosea Taifa na pia haukutumia akili

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ali D’amoush, Rais wa Baraza la Utendaji la Hizbullah, amesisitiza kwamba uamuzi wa kijinga ambao serikali imechukua wa kutaifisha silaha za Muqawama si tu kwamba si tu kwamba umekosea sehemu ya kanuni, bali pia umelikosea Taifa na pia haukutumia akili.

Ameongeza: Inawezekanaje nchi ambayo ardhi yake imevamiwa na adui, inashambuliwa kila siku, wananchi wake wanazuiwa kurejea vijijini na majumbani mwao, na raia wake wametekwa na adui, serikali yake ichukue uamuzi wa kuondoa moja ya vipengele muhimu zaidi vya nguvu zake, yaani Muqawama?

Sheikh D’amoush ameendelea: Serikali isiyoweza kulinda wananchi wake dhidi ya adui dhalimu kama Israeli, inawezaje katika kilele cha mapambano kuondoa silaha za harakati ya muqawama? Je, huu siyo ukengeufu kutoka kwenye mantiki, akili na maslahi ya kitaifa?

Amesisitiza kuwa: Mantiki, akili na maslahi ya kitaifa yanasema: ikiwa nchi ina nyenzo za nguvu, jukumu lake la kwanza ni kuzilinda hizo ili inufaike nazo.

Mjumbe mwandamizi wa Hizbullah amesema: Tunayo serikali ambayo inatekeleza maslahi ya nguvu za kigeni, serikali na maagizo yao, si serikali inayoweka maslahi ya watu na jamii yake mbele, uamuzi wa serikali ni hatari na hatujui matokeo yake, uamuzi huu unaweza kuliweka taifa katika ukingo wa mlipuko na serikali inalazimika kuufuta.

Sheikh D’amoush ameashiria kuwa: Kwa uamuzi huu wake, serikali imegeuza tatizo na adui Muisraeli kuwa tatizo la ndani miongoni mwa Walebanoni, na hivyo kufungua njia ya mwelekeo wa ndani uliojaa hatari, vurugu na matatizo, ni kweli kwamba Walebanoni wanatofautiana kisiasa juu ya masuala mengi, lakini uamuzi wa serikali umezidisha tofauti hizi na kuwafarakanisha Walebanoni, ilhali jukumu la serikali ni kuwaleta pamoja, siyo kuchimbua zaidi migawanyiko yao.

Amesema: Leo, Muqawama ni kielelezo cha utambulisho wa kitaifa na kijamii na ni alama ya kijihadi iliyojengwa kwa damu, kujitolea na mashahidi, hakuna mtu anayeweza kuifuta au kuondoa silaha zake kwa uamuzi au taratibu fulani kana kwamba ni jambo la kiufundi au kisanii tu.

Mjumbe wa Baraza Kuu la Hizbullah amesisitiza kuwa: Muqawama ni utambulisho, ni tamaduni, ni uhusiano, ni tendo la kiimani na kiitikadi, ni kipengele kamili cha kitaifa chenye kazi ya kitaifa, silaha zake si silaha za vikundi vya wanamgambo zilivyotumika kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe, wala si silaha zisizo na utaratibu ambazo zinaweza kusemwa ni silaha dhidi ya taifa

Ameendelea kusena: Silaha wanazozizungumzia ndizo zilizoikomboa sehemu kubwa na ya thamani ya ardhi yetu, ndizo zilizokabiliana na uvamizi kwa miongo minne iliyopita, ndizo zilizoilinda Lebanon, zikamshinda adui na zikazuia uvamizi wa Lebanon.

Sheikh D’amoush amesisitiza kuwa: Silaha ambazo vita vyote vya Israeli havikuweza kuziondoa wala kuziharibu, Silaha hizi zitaendelea kuwepo maadamu kuna uvamizi na dhulma, hakuna mtu anayepaswa kuwekeza matumaini katika udhaifu wake, mtu yeyote anayebeti juu ya udhaifu wake kutokana na mabadiliko ya kieneo na kimataifa, anakosea na yuko kwenye udanganyifu.

Mjumbe mwandamizi wa Hizbullah amebainisha kwsmba: Hatutaingia kwenye mjadala wowote juu ya utekelezaji wa uamuzi wa serikali; kwa sababu hatuutambui na hautuhusu  hakutakuwa na mazungumzo yoyote kuhusu silaha kabla ya kuondoka Israeli na kusimamisha uvamizi wake dhidi ya Lebanon, wote wanapaswa kufahamu kuwa Muqawama hautapoteza uhalali wake, si kwa uamuzi wa serikali, si kwa karatasi yoyote ya Marekani.

Amesisitiza kuwa: Muqawama unapata uhalali na haki yake kutoka kwenye matakwa ya watu na maslahi halisi ya taifa na jamii yake, kwa mujibu wa kura za maoni, Muqawama licha ya kampeni zote za uchochezi, shaka na upotoshaji wa kisiasa na vyombo vya habari, bado ni chaguo la idadi kubwa ya Walebanoni.

Sheikh D’amoush ameongeza: Hadi sasa tumetenda kwa utulivu na hatujatumia hatua kubwa za maandamano, lakini mwenendo huu unaweza usiendelea kwa muda mrefu, kwa sababu ya wasiwasi juu ya uthabiti na kutoa nafasi kwa serikali kurekebisha uamuzi wake, hatujachochea hali, lakini iwapo serikali itang’ang’ania kupitisha uamuzi wake, huenda tukalazimika kufanya hivyo.

Mwisho amesema: Hali ya leo ni ya Karbalaa na Husayni, na tunawaambia wale Mayazidi wote wanaotuweka kati ya chaguo mbili za kujisalimisha au kupigana, maneno yale yale ambayo Imam Husayn (a.s.) alisema siku ya ‘Ashuraa:


 «ألا وإن الدعیّ ابن الدعیّ قد رکز بین اثنتین، بین السلّة والذلة وهیهات منا الذلة».

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha